January 15, 2019


Kabla hata hawajakipiga na As Vita katika Ligi ya Mabingwa Afrika, baadhi ya mashabiki wa klabu ya Simba wameutaka uongozi kucheza na Al Ahly saa 9 alasiri ili kuwapa wakati mgumu uwanjani.

Mashabiki hao ambao hawataki kabisa kuwasikia waarabu kutokana na tamaduni zao za kujiangusha na fitina uwanjani, wamewaomba mabasi chini ya Mwenyekiti wao, Swed Nkwabi, kuhakikisha ombi lao linatimizwa.

Hatua hiyo imekuja pia kutokana na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ambao Simba walicheza dhidi ya Al Masry mwaka jana kwenda sare ya mabao 2-2 Uwanja wa Taifa.

Sare hiyo imewakumbusha machungu Simba wakiamini kama mechi itapigwa mida hiyo kuna uwezekano Al Ahly wakapata mwanya wa kufanya vema.

Kabla ya kumenyana na Al Ahly, Simba itakuwa inacheza na AS Vita ya Congo Jumamosi ya tarehe 19 2019 wakati mechi ya kwanza na Al Ahly itachezwa Februari 1 2019.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic