January 15, 2019


Na George Mganga

Wakati kikosi cha Yanga kikitarajia kushuka dimbani leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC, mchezaji wake, Ibrahim Ajibu atakuwa anaweka rekodi ya kuanza kuvaa kitambaa cha unahodha mkuu.

Ajibu ambaye aliwahi kuichezea Simba ambayo ni bingwa mtetezi, atavaa kitambaa cha unahodha baada ya kukabidhiwa na Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera.

Ajibu alipewa kitambaa hicho huku Kelvin Yondani aliyekuwa akikitumia kupokwa kutokana na kuonesha utovu wa nidhamu kwa siku za hivi karibuni.

Zahera alisema aliamua kumvua unahodha Yondani kwa kuwa amekuwa utovu wa nidhamu na akisema liwe funzo kwa wachezaji wengine wa aina kama ya Yondani.

Yanga itakuwa inashuka kwa mara ya kwanza tena kusaka alama tatu katika ligi ikiwa ni baada ya michuano ya Mapinduzi CUP kumalizika huko Zanzibar.

Katika mashindano hayo Yanga ilitolewa baada ya kufungwa mabao 3-0 na Azam FC ambao walifanikiwa kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo kwa kuichapa Simba mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic