Matumaini ya kuupata mwili wa Emilio Sala yanaonekana kufifia baada ya mashabiki wa Cardiff City kuanza kuweka maua nje ya uwanja huo.
Sala raia wa Argentina anahusishwa kuanguka na ndege na iliyokuwa ikisafiri kutoka Ufaransa kwenda Cardiff.
Polisi ya Ufaransa imethibitisha kwamba Sala ambaye alitua Cardiff baada ya KRC Genk kukataa kumuuza mshambuliaji wake, Mbwana Samatta alikuwa kwenye ndege hiyo.
Ndege hiyo ilitoweka kwenye rada karibu na kisiwa jirani kabisa na Wales na inaelezwa ndege hiyo ilikuwa na abiria wawili.
Imeelezwa ndege aliyokuwamo ilikuwa njiani kwenda Cardiff na Sala alikuw amejipanga kuanza kazi yake hiyo mpya.
Baada ya kusaini mkataba kwa kitita cha pauni milioni 15, Sala alirejea Nantes nchini Ufaransa na kuwaaga wachezaji wenzake huku akikamilisha masuala kadhaa ya kifamilia.
Ujumbe wake wa mwisho kwenye Mtandao wa Kijamii wa Twitter, aliwaaga wote waliokuwa pamoja, kumuunga mkono na kadhalika kwa kuwa alikuwa anakwenda kuanza kazi mpya.
0 COMMENTS:
Post a Comment