January 22, 2019





Yanga imeanza kwa kuyaaga mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kuchapwa kwa mabao 3-2 lakini Kocha wake Mwinyi Zahera amesema uchovu wa Ligi Kuu Bara, umechangia.

“Mechi zipo karibu sana, tumetoka Shinyanga na kufikia mazoezi halafu mechi. Ukingalia hawa hata hawakufanya jambo kwa karibu siku nne,” alisema Zahera raia wa DR Congo.

“Lakini hiyo bado siwezi kufanya kama kisingizio, najua hapa watasema najitetea lakini ni uhalisia. Tumetoka na tuwapongeze walioshinda.”

Kariobang kutoka Kenya waliongoza hadi mabao 2-0 wakati wa mapumziko. Yanga walipata bao kupitia Amissi Tambwe lakini Wakenya hao wakaongeza bao la tatu.

Yanga walifunga bao dakika za mwisho kabisa na kufanya iwe 3-2, juhudi za kusawazisha zikapamba moto, hata hivyo haikuwezekana.

11 COMMENTS:

  1. Jana aliorodhesha mataji ambayo ana uhakika wa kuyachukua. Aliyataja makombe matatu [3] (SportsPesa, Ligi kuu na FA).

    Kwenye maoni ya wasomaji humu, kuna mmoja ali"comment" - "Hakuna hata kombe moja ambalo Yanga mtachukua".

    Dalili hizo zimeanza kuonekana leo, Kombe mojawapo kati ya matatu ambayo yapo kwenye mipango ya Kocha wa Yanga, limeshaponyoka, sijui mengine hayo mawili.

    Kingine, kocha usianze kuleta sababu za mechi kuwa karibu karibu ndo sababu ya kufungwa, sasa ukirudi kwenye ligi ambako utakuta ratiba kila baada ya siku mbili ya tatu unacheza mechi, si ndio itakuwa wimbo wa Taifa na kuanza kutafuta mchawi hapo!. Jipange Papaaaaa Zahera, Hii ndio ligi ya Bongo, hakuna vya laini laini huku.

    ReplyDelete
  2. Mmechoka wapi wakati mapinduzi cup hamkucheza...Simba ilicheza Siku tatu mfululizo na bado walifanya vema...sasa taendelea kutembeza kopo!Zanzibar hujapata kitu na hapa sportpesa pia

    ReplyDelete
  3. Yanga harakisheni uchaguzi au muunde Kamati ya Kusimamia Timu kimaslahi na Nidhamu....kwani mnapoelekea nidhamu inapungua ndani ya Timu

    ReplyDelete
  4. Kocha wa Yanga hana mbinu anaongea sana na vyombo vya habari badala ya kujikita kukisuka kimbinu timu yake.....watu wanaaminishwa ubora wa timu lakini kiuhalisia beki mbovu sana hata golikipa hawana formation ya kucheza kwa mbinu....Kocha msanii sanii tu Kombe hili anachukua Simba au Gor Mahia. Yanga wasipofanya mageuzi katika beki na viungo vyao jinsi wanavyocheza na kukaba pindi wanapoteza mpira wataendelea watapoteza mechi nyingi....KAMA NI MDAU WA YANGA UNASOMA UJUMBE HUU FIKISHA KWA HARAKA SANA UJUMBE KWA KOCHA

    ReplyDelete
  5. Visingizio tu.Hamna plan B Tukikutana na timu nzuri tutafungwa goli 7.

    ReplyDelete
  6. Ana2zingua 2 huyo hanajipya kazi yake anayoijua kuweka mabifu nawachezaji 2

    ReplyDelete
  7. Na bado! Mbona ndo kwanza mawio haya!.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic