Nahodha msaidizi wa timu ya Yanga, Juma Abdul amesema kuwa kikosi cha Simba kitakutana na upinzani kwa waarabu kutokana na namna walivyo na kasi katika ushambuliaji hivyo wanapaswa kuwa makini.
Abdul amesema kuwa michezo ya kimataifa huwa inakuwa na ushindani mkubwa hasa kutokana na kila timu kujipanga vizuri hivyo asili ya waarabu wengi wanapenda kutumia viungo na mashambulizi ya kasi.
"Waarabu muda wote wakiwa nyumbani ama ugenini hupenda kushambulia kwa kasi na kutumia viungo wao katika kutengeneza mashambulizi hivyo Simba wanapaswa wawe makini.
"Ubovu wao mara nyingi huwa sehemu ya ulinzi ila inabebwa sana na kufichwa na viungo wao sasa ili waweze kupata matokeo inabidi walazimishe kupata matokeo mapema na wawe imara kwa upande wa ulinzi, nina imani watafanya vizuri wakijipanga," alisema Abdul.
Simba wapo Kundi D katika Ligi ya Mabingwa ambalo lina timu kama JS Saora ya Algeria, Al Ahy ya Misri na AS Vita ya Congo leo wataanza kazu dhidi ya JS Saoura Uwanja wa Taifa.
Kuna siri moja au mbinu muhimu wanazozitumia timu kutoka Africa ya kasikazini kuzimaliza timu zetu na mara nyingi hufanikiwa kana kwamba vile wanaambizana. Nayo ni kutafuta magoli ya mapema hasa ndani ya dakika ishirini za mwanzo za mchezo ili kuwachanganya. Unakumbuka Simba ilivyofungwa na Almasry ni mbinu ile ile. Inaonekana hata Nkana FC walitumia mbinu hiyo hiyo sema tuwe wa kweli Simba kule mbele wapo vizuri kuwazuia wasipate japo goli moja basi hiyo timu lazima itakuwa imejipanga hasa. Nilimuliza rafiki yangu kutoka Ethiopia kwanini huwa mara nyingi timu zao huwa wanazisumbua sana timu za kiarabu hasa za Misri akaniambia siri moja kubwa za kuzimaliza timu za kiarabu ni kujipanga na kupambana piga Uwa kuhakikisha hawapati bao katika dakika za mapema hasa dakika ishirini za mwanzo za kipindi cha kwanza na dakika ishirini za kipindi cha pili baada ya kutoka mapumziko.Na kama kuna timu katika ukanda wetu huu wa karibu warabu wanachukia kwenda kucheza basi ni kupangwa na timu za Ethiopia kwani mara nyingi huwa wanachemka. Tatizo kubwa kwa timu zetu wanapoingia uwanjani kuanza mpira mara nyingi wachezaji huwa kama vile mtu aliekurupushwa kutoka usingizini mara nyingi huwa hawajielewi,huwa hawapo tayari mpaka wakesha fanya makosa ndio wanaamka lakini siku zote huwa too late hasa kwa timu za warabu wakikufunga goli la mapema huwa kama fisi alieonja damu ya mnyama waliemjeruhi lazima watammaliza tu, ikiwezekana wakupige bao la pili haraka haraka wakuchanganye zaidi halafu wamalizie kwa kujiangusha hovyo ikiwezekana hata kumtafutia mtu kadi nyekundu. Kwa hivyo wahusika waliokuwepo karibuni na wachezaji wa Simba lazima wawasisitize wachezaji kukomaa kabisa kuhakikisha hawawapi warabu nafasi ya kufunga hasa goli la mapema licha ya mipango ya timu kwa mechi ya kwsho kushambulia zaidi. Na wachezaji wa viungo wa Simba hasa kiungo cha chini lazima awe sharp zaidi kupambana kabla mpira hauja wafikia mabeki. Kwenye kiungo cha chini ndiko kwenye uozo wa backline ya Simba kwa hiyo lazima kurekebishwe.
ReplyDelete