Imeripotiwa kuwa serikali imeyafuta mashamba sita (ekari 12,915.13) ya Mohammed Enterprises Limited (MeTL).
Serikali imefuta leseni ya mashamba hayo yaliyopo Korogwe jijini Tanga, kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu.
Taarifa imesema kwa mujibu Naibu Waziri Angeline Mabula amesema uamuzi huo unalenga kuhakikisha wenye rasilimali za serikali wanafuata masharti.
Waziri ameeleza kuwa kuwepo kwa mashamba hayo ambayo yamekuwa hayafanyiwi kazi yoyote ni tofauti na matakwa ambayo yaliwekwa hapo awali.
Waziri amesema wmefikia maamuzi hayo kutokana na kumtaka mmiliki mkuu wa mashamba hayo hapo awali kuyaendeleza lakini haikuwa hivyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment