January 19, 2019



KOCHA Mkuu wa AS Vita ya Congo, Flolent Ibenge amesema hajapata nafasi ya kuwaona wapinzani wao namna wanavyocheza na mbinu zao kutokana na kuzimwa kwa mitambo inayoruhusu mtandao maarufu kama intaneti.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeamua kuzima mitambo hiyo kutokana na masuala ya usalama nchini hapo baada ya kufanyika uchaguzi mkuu, baada ya kutangazwa kwa Felix Tshisekedi kuwa mshindi kumekuwa na mapingamizi kadhaa hasa la mgombea mwenzake Martin Fayulu aliyeshika nafasi ya pili kuamua kufungua kesi.

Ibenge amesema kutokana na tatizo hilo ameshindwa kupata muda wa kuwatazama wapinzani wake kwa ukaribu hali inayomfanya aingie Uwanjani akiwa hajatambua mbinu za wapinzani wake.

"Sijapata muda wa kuwatazama wapinzani wangu, mtandao huku unasumbua sana ndio maana mambo mengi yanashindwa kwenda kwa wakati, ila hilo sio tatizo kubwa wachezaji wangu watafanya kazi Uwanjani kutafuta ushindi, nawaheshimu wapinzani tutapambana kupata matokeo," alisema Ibenge. 

Simba anacheza leo mchezo wake wa kwanza ugenini kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wake wa kwanza nyumbani.

3 COMMENTS:

  1. Brother leo utafungwa 3-0 na baada ya kufungwa mtandao utafanya kazi.Simba is the big brand

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nadhani utakuwa umeshaelewa nani ni big brand...maana kipigo mlichopata huko si mchezo..5G

      Delete
    2. Brand pale na Manara tu wengine wanafuga ndevu tu...

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic