January 19, 2019


KOCHA wa Mwadui FC, Ally Bizimungu amesema wana kazi kubwa ya kufanya leo mbele ya wapinzani wao Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ugenini kutokana na ushindani uliopo.

Mwadui watakuwa ugenini leo wakicheza na Azam FC Uwanja wa Chamazi wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare mchezo wao wa kwanza mzunguko wa kwanza.

Bizimungu amesema kikosi chake kipo sawa kwa ajili ya mchezo wao wanatarajia kupata ushindi licha ya kutomtumia mchezaji wao Ditram Nchimbi ambaye walimchukua kwa mkopo kutoka Azam FC.

"Tutashuka Uwanjani kushindana kwenye mchezo wetu wa leo licha ya kutomtumia Nchimbi kutokana na utaratibu wa TFF kutoruhusu wachezaji wa mkopo kuchezea timu walizotoka ila tumejipanga kupata matokeo," alisema Bizimungu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic