WAPINZANI wa Simba kwenye mashindano ya SportPesa Cup AFC Leopards ya Kenya wamewasili leo nchini Tanzania kwa ajili ya kumenyana na Simba Januari 23.
Mashindano hayo yanashirikisha timu nane ikiwa ni nne kutoka Tanzania na nne kutoka Kenya ambazo ni Simba, Mbao FC, Yanga na Singida United kwa Tanzania na Gor Mahia, AFC Leopards, Kariobang Sharks na Bandari kutoka Kenya.
Bingwa wa mashindano haya atapata fursa ya kucheza na timu ya Everton na bingwa mtetezi ni Gor Mahia ya Kenya ambao ni washindi wa kombe mara mbili mfululizo.
0 COMMENTS:
Post a Comment