MWANA FA: HATA WAJE BARCELONA KWA SIMBA HII HAWATOKI
Mkali wa michano Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, ameungana na msemaji wa Wekundu wa Msimbazi, Haji Manara, kusema kwamba hata Barcelona wakija Dar kwa Simba hii wanaacha pointi tatu.
MwanaFA ambaye ni shabiki wa kutupwa wa Simba, amefikia kutoa kauli hiyo baada ya juzi timu yake kuichabanga JS Saoura ya Algeria kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika.
Lakini kabla ya mchezo huo, Manara alisema kuwa kwa Simba hii, hata wangepangwa na Bayern Munich ya enzi zile, Barcelona ya akina Xavi na Manchester City, lazima washinde Uwanja wa Taifa.
Kwa mujibu wa Championi Jumatatu FA alisema kwenye kundi lao hakuna timu itakayoisumbua Simba kwa sababu kikosi chao kimeimarika mara tano ya kilivyokuwa awali, hivyo levo yao kwa sasa ni kucheza dhidi ya Barcelona au Bayern na siyo vitimu vidogo kama JS Saoura.
“Wale walikuwa wanakufa saba na siyo tatu, we si umeona Pascal Wawa alichokuwa anakifanya, ulimuona James Kotei? Kwa hiyo ile ndiyo Simba.
“Sasa hivi inatakiwa tupangiwe na Barcelona na Bayern Munich na siyo vitimu hivi vya ajabuajabu, ni kutuvunjia heshima,” alisema FA.
Niko na wewe Brother.Simba is the Big Brand.
ReplyDeleteWale waarabu hawana tofauti na Prisons ya Mbeya,wote wapo nafasi ya 4 toka mkiani.
DeleteWako nafasi ya tano bro cheki vizuri msimamo
DeleteSasa wabongo wameigeuzia kibao Js Soura kuwa ni kibonde wa kundi D kisa kufungwa na Simba? Tena wanao iita Soura kibonde ni wale wachambuzi wanaojiita wana macho ya jini yenye uwezo wa kuona visivyoonekana na macho ya kawaida? Kama Soura angefungwa na Ahly hata Goli sita bila shaka asingekuwa kibonde? Utaona jinsi gani watanzania tusivyozithamini juhudi zetu. Ikiwa hao wanaojiita wachambuzi mahiri bado wangali wana mawazo mgando ya yakwamba sisi ni kupigwa tu vipi mshabiki mjinga wa kawaida? Vipi ikitokezea Js Soura akampiga Ahly? Nadhani watarudi tena kusema Simba alibahatisha kwa Soura. Wakati mwengine kuwa mtanzania ni shida tupu lakini ndio basi tena.
ReplyDeleteInaboa sana nijaribu kufikiri na kishangaa kwa mfano huyu shafii macho makavu na anendelea kusisitiza hivi mpira wa soka unachezwachumbani ukimtazama kwwa makini haipendi simnba sasa huyu ni mchamnuzi au maujanja?inasikitisha sana asanteni sana mkde na jeshi lako kwa mwanzo mzuri na patrick uchebe najua hizi ni rasha rasha masika yanakuja
ReplyDelete