January 13, 2019


Ni kivumbi cha Simba Queens na Yanga Princess leo Jumapili kwenye Ligi Kuu ya Wanawake. Makocha wa timu hizo wametambiana kila mmoja kuondoka na ushindi katika mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, kiingilio kikiwa buku 2 tu.

Kocha wa Simba, Omary Mbweze, alisema: “Simba tumejipanga vizuri kushinda kila mechi, tayari nimewaona Yanga na ninajua mapungufu yao, lakini siwezi kuwadharau zaidi nahitaji pointi tatu.”


Kwa upande wa Kocha wa Yanga, Hamis Kinonda, alifunguka kuwa: “Lengo ni sisi kushinda ingawa tumekuwa tukipambana licha ya ugeni kwenye ligi, tunajua wenzetu wana wachezaji wenye uzoefu tofauti na sisi, lakini tutapambana kupata ushindi.”

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Soka la Wanawake, Amina Karuma, alisema wamejipanga na ulinzi utakuwa wa kutosha pamoja na burudani zikiongozwa na wadhamini wao Serengeti Lite, hivyo mashabiki wajitokeze kushuhudia mchezo huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic