January 13, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga umeutolea ufafanuzi ujumbe wa kiungo wake Mzimbambwe, Thaban Kamusoko baada ya kuleta sintofahamu kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kamusoko hivi karibuni aliandika ujumbe huo ukieleza kuwashukuru wapenzi na mashabiki wa Yanga kwa upendo waliomuoneshea tangu ajiunge na timu hiyo.

Kamusoko aliandika ujumbe huo ambapo mashabiki wengi waliokomenti walielewa kuwa ameshaagana na mabosi wake na ikachukuliwa kuwa anaondoka Yanga.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari, Dismas Ten, ameibuka na kuutolea ufafanuzi kuwa Kamusoko aliandika na hakuwa na maana ya kuondoka.

Ten ameeleza kuwa ifikie wakati mashabiki wasiwe wanakariri mambo pale mtu anapoandika ujumbe wa aina kama ile, kwani si kweli kuwa anaondoka.

"Si kweli, alichokiandika hakina maana ambayo wengi wametafsiri, bado ana mkataba na Yanga na ataendelea kuwepo" alisema Ten.

4 COMMENTS:

  1. wewe c ndo uliandika kuwa ameondoka au nani

    ReplyDelete
  2. Sio mashabiki ni wewe mbumbumbu unayependa kujiandikia mradi ufaidike sijui umetumwa kuivuruga Yanga

    ReplyDelete
  3. Mashabiki wa Yanga mnaidhalilisha nchi kushangilia wageni ni mara mia bora mkaae nyumbani kuliko kuja uwanjani na kushangilia mwishoni aibu inawakuta Simba itashinda tu....huu ni mkakati (TFF, Simba wanachama, wageni, Serikali kuu, serikali ya mkoa na Jeshi la Polisi na wadhamini au wawekezaji wa klabu ya Simba) pointi 9....kwa mchina lazima....nguvu moja....ni kauli mbiu kwa vitendo....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic