MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Simba, Emmanuel Okwi amesema alikuwa anashindwa kuonyesha kiwango cha juu kutokana na kusumbuliwa na maumivu yaliyokuwa yanamfanya ashindwe kuonyesha makeke Uwanjani.
Okwi alifanikiwa kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao matatu mbele ya waarabu JS Saoura ya Algeria baada ya kufunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao.
"Kwa sasa nipo fiti na nitaendelea kupambana kwa ajili ya timu yangu, nilikuwa nashindwa kufanya vizuri kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mgongo ila kwa sasa maumivu yamekwisha ni mwendo wa kazi tu," alisema Okwi.
Simba watakuwa na kazi Jumamosi kuivaa AS Vita ya Congo kwenye mchezo wao wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment