KOCHA Mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kilichowaponza kupoteza pointi tatu ugenini ni mwamuzi kuzidiwa nguvu na mchezo wake wa jana dhidi ya Mbeya City kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Sokoine.
Katwila amesema walipambana kwa hali na mali kupata matokeo ila hakukuwa na utaratibu wa kufuata sheria 17 za mpira hali ambayo iliwafanya wapoteze mchezo wao.
"Tumecheza kwa kujituma na juhudi kubwa tumeonyesha, kipindi cha kwanza tulikwenda sawa ila kipindi cha pili mwamuzi alizidiwa na kelele hali ambayo imefanya tupoteze, ila haina namna siwezi kumlaumu mwamuzi kwani kuna kamati ya kumhukumu na sio mimi," alisema Katwila.
Katwila anaziacha pointi sita mkoani Mbeya kwani alianza kupoteza mbele ya Tanzania Prisons na jana akapoteza mbele ya Mbeya City.
0 COMMENTS:
Post a Comment