RAMSEY, DYBALA, ARSENAL, BENITEZ: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO
Arsenal wanaweza kumruhusu kiungo wake raia wa Wales Aaron Ramsey, 28, kujiunga na miamba ya Italia Juventus mwezi huu iwapo watawanasa kwa mkopo nyota wa Barcelona Denis Suarez, 25, na nyota wa Real Madrid James Rodriguez, 27, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo katika klabu ya Bayern Munich. (Independent)
Real Madrid wanaandaa kitita cha pauni milioni 90 kumsajili katika majira ya kiangazi mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 25. (Sun)
Kocha Rafael Benitez anatarajiwa kuachana na klabu yake ya Newcastle United mwishoni mwa msimu endapo wachezaji wawili anaowataka wasisajiliwe katika majira haya ya baridi. (Telegraph)
Kiungo wa Atlanta United raia wa Paraguay Miguel Almiron, 24, ndiye chaguo la kwanza la usajili kwa Benitez. (Mirror)
Newcastle pia wametangaza dau la pauni milioni 4.3 ili kumsajili winga raia wa Ureno Gelson Martins, 23, anayekipigia Atletico Madrid kwa mkopo. (AS - in Spanish)
Manchester United wanakabiliana na ushindani kutoka Tottenham katika harakati za kumsajili winga raia wa Uholanzi Steven Bergwijn, 21, anayechezea klabu ya PSV Eindhoven. (Sun)
Paris St-Germain wametangaza nia ya kumsajili kiungo wa Everton raia wa Senegal Idrissa Gueye, 29. (L'Equipe - in French)
Everton wanaweza kukubali kitita cha pauni milioni 40 kutoka PSG ili wawauzie Gueye, sehemu ya kitita hicho itasaidia klabu hiyo kutoka jiji la Liverpool kumnasa mshambuliaji mpya. (Mirror)
Mchambuliaji wa Italia Mario Balotelli, 28, amekubali kujiunga na klabu ya Marseille kwa mkataba wa miezi sita akitokea klabu nyengine ya Ligue 1 Nice. (L'Equipe, via Mail)
Chelsea inakabiliana na ufinyu wa muda katika harakati za kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Argentina na Juventus Gonzalo Higuain, 31, endapo wanataka mchezaji huyo aingie dimbani kwenye mechi yao dhidi ya Tottenham kesho Alhamisi kwenye nusu fainali ya pili ya michuano ya kombe la Carabao. Higuain kwa sasa yupo AC Milan kwa mkopo. (Mail)
Beki wa kushoto wa Manchester City Benjamin Mendy, 24, anatarajiwa kurejea kikosini leo Jumatano katika mechi ya nusu fainali ya pili dhidi ya Burton baada ya kupona majeraha yake ya goti. (Independent)
Kocha Pep Guardiola anatazamiwa kuanzisha wachezaji watato kutoka kikosi cha makinda wa Manchester City katika mechi ya leo, hii inatokana na ushindi mzito wa 9-0 dhidi ya Burton walioupata kwenye nusu fainali ya kwanza. (Manchester Evening News)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment