January 23, 2019


Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi nchini, Steven Mguto, amesema sababu ya ligi kuwa na mechi nyingi za viporo ni kutokana na muingiliano wa mashindano.

Mguto ameeleza kuwa viporo hivyo haswa vimechangiwa na uwepo wa mashindano makubwa barani Afrika, Ligi ya Mabingwa ambayo Simba wanashiriki hivi sasa.

Ameeleza wanajitahidi kwa kadri wanavyoweza kuhakikisha viporo hivyo wanachezeka ili kuiweka ligi sawa na imalizike kwa wakati.

Mguto amesema Simba bado ipo kwenye mashindano ya kimtaifa na hii inapelekea kubadilika kwa mechi kila wakati na kusababisha kuwe na viporo.

Mbali na Mguto, wadau wengi wa soka nchini wamekuwa wakihoji kwanini ligi inakuwa na viporo vingi na kila siku kumekuwa na panga pangua ya mechi jambo ambalo linaifanya ligi kuwa dhaifu.

1 COMMENTS:

  1. Daah ni ajabu na kweli...
    Kwa hiyo hawana imani na timu kama #Simba au ndo kusema kuwa hawakutegemea #Simba kufika mbali hivyo kwenye mashindano ya kimataifa..!!??

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic