January 14, 2019



BONDIA mstaafu Rashid Matumla maarufu kama 'Snake Boy', ambaye alipata kuwika miaka ya 1996 na alipata heshima ya kuitwa Ikulu na rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, amesema kuwa ili kuweza kufikia mafanikio makubwa kwa mchezo wa ngumi, kuna ulazima wa serikali kuanzisha vituo maalumu vya kuibua vipaji.

Matumla ambaye alianzisha kituo cha kuibua vipaji katika Kitongoji cha Mbagala, ameshindwa kuendeleza kituo hicho kutokana na kukosa vifaa kwa sababu ya gharama kubwa ya kuendesha.

Ameiomba serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyo chini ya Dk Harrisson Mwakyembe, iwakumbuke wastaafu pia.

"Tuna uwezo mkubwa wa kuwafundisha vijana ambao wana vipaji vya kupiga masumbwi wakiwa uwanjani ila tatizo kubwa lililopo kwa sasa ni vifaa vya kutendea kazi kwani huwezi kumfundisha kijana awe bora katika mazingira yasiyo rafiki.

"Wakati wa kuwekeza kwa vijana ni sasa, makocha wa ngumi na wale wenye ujuzi wa kupigana, wakipewa nafasi ya kuwa kwenye kamati za mashindano na kupewa sapoti ya kutosha kwa upande wa vifaa tutafika mbali kwa kuibua vipaji vingi," alisema Matumla.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic