MABINGWA wa kihistoria wa Tanzania Bara, Yanga wamesema wamejipanga kiasi cha kutosha kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui utakaochezwa kesho Uwanja wa Taifa.
Yanga wanaanza mzunguko wa pili wakiwa na mchezo mmoja wa mzunguko wa kwanza mkononi dhidi ya Azam FC.
Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kikosi kipo sawa na kilianza mazoezi muda mrefu kuwawinda wapinzani wao Mwadui FC.
"Kikosi kipo sawa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mwadui, morali waliyonayo wachezaji ni kubwa na wanatambua wana kazi kubwa ya kufanya ili kupata pointi tatu, tunachohitaji ni kupata matokeo chanya.
"Hatuna majeruhi mpaka sasa hivyo kazi kubwa iliyobaki ni kwa wachezaji wenyewe kufanya kile ambacho mwalimu amewafundisha, mashabiki watupe sapoti," alisema Ten.
Yanga wamecheza michezo 18 na wamefanikiwa kushinda michezo 16 na kupata sare michezo miwili wanaongoza Ligi wakiwa na pointi 50.
0 COMMENTS:
Post a Comment