SINGIDA SASA KUPIGA SOKA LA KISERBIA TU, YAMALIZANA NA MAKOCHA WAWILI
Uongozi wa klabu ya Singida United umeamua kuvunja benki kwa kuwasajili Makocha wawili kutoka Serbia kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo.
Popadic Dragan ambaye ni Kocha Mkuu ameamua kuja na mwenzake ambaye atakuwa Msaidizi, Dusan Momcilovic.
Usajili wa makocha hawa umefanikiwa ikiwa ni baada ya klabu hiyo kutokuwa na Kocha Mkuu tangu kuondoka kwa Hans Van Der Plujim ambaye alitimkia Yanga.
Pengine Singida wameamua kuboresha benchi la ufnudi kwa ajili ya michuano ya SportsPesa Super CUP itakayokuja hivi karibuni.
Huko walipokwenda Singida kutafuta makocha wamepatia hasa ndiko kwenye wanaume wa shoka katika kazi za ukocha ila kama Singida watamudu kuwatunza hao makocha kwa sababu tunasikia wachezaji wanalia njaa vipi wataweza kuwahudumia makocha wa kigeni?
ReplyDelete