KOCHA Mkuu wa Azam FC, Mholanzi Hans Pluijm amewataka nyota watakaoanza leo dhidi ya JS Saoura katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa kutafuta matokeo haraka.
Pluijm ambaye alifanikiwa kuifundisha Yanga na kuifikisha hatua ya makundi ya Shirikisho amesema kikubwa ambacho wachezaji wa Simba wanatakiwa kukifanya ni kulinda pumzi yao iwe ya kutosha na kutafuta mabao ya mapema.
"Nipo Zanzibar kwa sasa nimepata bahati ya kuona kikosi cha Simba kikiwa Uwanjani, wana wachezaji wazuri na bora hasa linapokuja suala la kutafuta matokeo hivyo wanachotakiwa kuboresha ni kulinda pumzi yao isikate mapema na kutafuta ushindi wa mapema Uwanjani.
"Wachezaji wao wengi wana uwezo na uzoefu na mechi za kimataifa, Kagere, Okwi, Chama, Wawa sasa hawa wasicheze wao wenyewe bali wacheze wakiwa ni timu hapo ndipo watapata matokeo ambayo wanayataka, hakuna haja ya kuwa na hofu kila kitu kinawezekana," alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment