January 22, 2019

TIMU ya Singida United ya Tanzania imepoteza mchezo wake wa le wa hatua ya robo fainali kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Bandari uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Singida United imepoteza mchezo huo na inakuwa ni timu ya kwanza kuondolewa kwenye hatua ya robo fainali kutoka Tanzania na kuifanya Bandari kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali.

Mchezo unaoendelea kwa sasa ni kati ya Yanga na KK Sharks Uwanja wa Taifa ili kumpata mshindi atakayetinga hatua ya nusu fainali ya mashindano haya.

Mshindi wa SportPesa Cup atapata fursa ya kucheza na timu ya Everton ambayo nayo inadhaminiwa na kampuni ya SportPesa na msimu huu mshindi atafuatwa nyumbani na Everton wenyewe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic