January 12, 2019


Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe amewapa mchongo Simba kuelekea mechi yao ya leo dhidi ya JS Saoura ya Algeria itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tambwe ambaye amewahi kuichezea Simba miaka ya nyuma, amewataka Simba kutokuwa na hofu ya timu hiyo na badala yake waingie uwanjani wakiwa na lengo moja tu la kupata ushindi.

Alisema kama wanahofu ya kufanya vibaya basi waachane nayo mara moja na kujaa matumaini ya ushindi katika mchezo huo jambo ambalo linaweza kutimia.

“Naamini watafanya vizuri kutokana na ubora wa kikosi chao kwa sasa. Wakiwa uwanjani hawatakiwi kuwa na hofu, wanapaswa kujiamini kwani hiyo ni silaha nzuri ya ushindi,” alisema Tambwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic