January 12, 2019


Singida United iko kwenye mazungumzo ya mwisho na Mserbia, Goran Kopunovic aliyewahi kuinoa Simba. Kocha huyo mwenye mbwembwe ataanza kazi kwenye mechi ya pili ya michuano maarufu ya SportPesa inayoanza Januari 22 Jijini Dar es Salaam. Mechi ya kwanza itakuwa dhidi ya Bandari.

Katika siku zilizobaki, Seleman Jabir na Shadrack Nsajigwa ‘Fusso’ ndio watakaokuwa na timu hiyo baada ya Mzanzibar, Hemed Morocco kuachana nao kutokana na ishu za masilahi. 

Habari za ndani zinasema kwamba Goran ambaye aliondoka Simba msimu wa 2014/15 ndiye chaguo la uongozi na wameshaafi kiana mambo mengi.

Habari zinasema kwamba wameamua kubadili benchi lote la ufundi kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo licha ya kwamba uchumi wao umedorora. 

Ingawa viongozi wa Singida wanafanya siri na jana hawakutaka kufafanua ishu hiyo, lakini inasemekana kwamba ishu imeiva na jamaa anatua muda wowote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic