Yanga imeanza kwa kuyaaga mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kuchapwa kwa mabao 3-2 lakini Kocha wake Mwinyi Zahera amesema uchovu wa Ligi Kuu Bara, umechangia.
“Mechi zipo karibu sana, tumetoka Shinyanga na kufikia mazoezi halafu mechi. Ukingalia hawa hata hawakufanya jambo kwa karibu siku nne,” alisema Zahera raia wa DR Congo.
“Lakini hiyo bado siwezi kufanya kama kisingizio, najua hapa watasema najitetea lakini ni uhalisia. Tumetoka na tuwapongeze walioshinda.”
Kariobang kutoka Kenya waliongoza hadi mabao 2-0 wakati wa mapumziko. Yanga walipata bao kupitia Amissi Tambwe lakini Wakenya hao wakaongeza bao la tatu.
Yanga walifunga bao dakika za mwisho kabisa na kufanya iwe 3-2, juhudi za kusawazisha zikapamba moto, hata hivyo haikuwezekana.
Kocha wa Yanga hana mbinu anaongea sana na vyombo vya habari badala ya kujikita kukisuka kimbinu timu yake.....watu wanaaminishwa ubora wa timu lakini kiuhalisia beki mbovu sana hata golikipa hawana formation ya kucheza kwa mbinu....Kocha msanii sanii tu Kombe hili anachukua Simba au Gor Mahia. Yanga wasipofanya mageuzi katika beki na viungo vyao jinsi wanavyocheza na kukaba pindi wanapoteza mpira wataendelea watapoteza mechi nyingi....KAMA NI MDAU WA YANGA UNASOMA UJUMBE HUU FIKISHA KWA HARAKA SANA UJUMBE KWA KOCHA
ReplyDelete