January 23, 2019


Kufuatia Ligi Kuu Bara kuwa na viporo vingi hivi sasa kumesababisha kila mdau na mpenzi wa soka aje na mawazo tofauti juu ya mwenendo mzima ulivyo.

Mchezaji wa zamani wa Yanga, Edibily Jonas Lunyamila, amesema kuwa ligi imepoteza mvuto kwasababu ya kuwa na viporo.

Amegusia kwa kuwataja Simba kuwa wna mechi za viporo nyingi japo akikiri kuwa ni kweli wanashiriki mashindano ya kimataifa na hakuna namna au haja ya kuwalaumu.

Lunyamila ameeleza kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linapaswa kujipanga namna ya kuifanya ligi iwe na ubora, walau kama ni viporo viwe viwili au vitatu.

"Unajua ligi yetu ni nzuri lakini kwa msimu huu imekuwa haina mvuto zaidi haswa kutokana na uwepo wa viporo vingi ambavyo vinapunguza ladha.

"Ingefikia hatua walau kuwe na viporo viwili ili kuifanya ligi iende sawa, sasa unakuta timu moja ina mechi nyingi, hili linasababisha kupotea kwa utamu wa ligi" alisema.

1 COMMENTS:

  1. Kocha wa Yanga hana mbinu anaongea sana na vyombo vya habari badala ya kujikita kukisuka kimbinu timu yake.....watu wanaaminishwa ubora wa timu lakini kiuhalisia beki mbovu sana hata golikipa hawana formation ya kucheza kwa mbinu....Kocha msanii sanii tu Kombe hili anachukua Simba au Gor Mahia. Yanga wasipofanya mageuzi katika beki na viungo vyao jinsi wanavyocheza na kukaba pindi wanapoteza mpira wataendelea watapoteza mechi nyingi....KAMA NI MDAU WA YANGA UNASOMA UJUMBE HUU FIKISHA KWA HARAKA SANA UJUMBE KWA KOCHA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic