KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Aussems amesema kuwa ameshindwa kubeba makombe matatu aliyoshiriki kutokana na kuweka nguvu nyingi kwenye michezo ya kimataifa.
Aussems amesema alihofia kuwaambia wachezaji wacheze kwa nguvu ili awalinde wasipate majeruhi kama ilivyotokea kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi.
"Nina michezo mingi migumu ikiwa ni pamoja na ule dhidi ya Al Ahly kwenye ligi ya mabingwa, nahofia nisije kupata majeruhi mwingine kama ilivyokuwa kwa Erasto Nyoni ambaye kwa sasa bado hajarejea Uwanjani.
"Sikupanga kubeba haya makombe matatu kwa kuwa hayapo kwenye hesabu zangu kikubwa ambacho nafikiria ni mchezo wangu wa Ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly," alisema.
Makombe hayo matatu ambayo amepishana nayo mbelgiji ni pamoja na lile la Mapinduzi, FA na kombe la SportPesa Cup ambalo limekwea pipa kwenda Kenya kwa KK Sharks.
0 COMMENTS:
Post a Comment