KOCHA Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems amewaondoa wachezaji wake watano katika michuano ya SportPesa Cup inayoendelea hapa nchini huku jina la nahodha, John Bocco likiwa la kwanza.
Simba, kesho inatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuvaana na AFC Leopards katika michuano hiyo.
Akizungumza na Saleh Jembe, Aussems amesema wachezaji hao amewaondoa kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya majeruhi.
Mbelgiji huyo aliwataja wachezaji hao ni Bocco, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe wote wenye majeraha, Asante Kwasi matatizo ya kifamilia ambaye yupo kwao Ghana na Yusuph Mlipili yeye amemuweka kando kwa sababu ya kiufundi.
“Sheria za SportPesa zinaruhusu kuwatumia wachezaji 22 pekee, hivyo kama kocha tayari nimependekeza wanajeshi wangu nitakaowatumia katika michuano hii.
“Vijana wangu wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo na wachezaji watano pekee ndiyo wanatarajiwa kuikosa michuano hii wakiongozwa na nahodha wetu Bocco, Kwasi, Nyoni, Kapombe na Mlipili,” alisema Aussems.
0 COMMENTS:
Post a Comment