January 12, 2019


Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ameendeleza kasi yake ya kukinoa kikosi chake katika Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar, tayari kuanza mechi yake ya mzunguko wa pili dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga ambapo ameweka mikakati ya kuhakikisha wanafanikiwa kuibuka na ushindi.

Yanga itashuka dimbani Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili huku wakiwa na kiporo cha mzunguko wa kwanza dhidi ya Azam FC mchezo ambao utapangwa baadaye.

Hadi sasa Yanga imefanikiwa kushinda mechi 16 kati ya 18 ilizocheza za mzunguko wa kwanza huku ikitoa sare michezo mwili na wana pointi 50.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omary Kaya alisema kuwa, kocha Mwinyi Zahera ameendeleza na mazoezi makali kwa ajili ya kuendeleza makali yao ya kutopoteza mchezo katika ligi kuu na wanataka kuingia kwa kasi kubwa raundi ya pili.

“Mazoezi yanaendelea vizuri, anachohitaji mwalimu ni ushindi tu ikiwezekana katika mechi zote za raundi ya pili.

“Tukimaliza mechi yetu ya Jumanne ndiyo tutafunga safari kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo dhidi ya Stand United,” alisema Kaya.

5 COMMENTS:

  1. sasa vipi hapo imezidi au imeipa simba maumivu? hivi unajitambua au huwa unafikiria wakati unaandika?

    ReplyDelete
  2. Hawa waandish wa Saleh Jembe hawapo makini na kazi yao. Kichwa cha habar hakifanani na maudhui zake

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na Waziri hawa waandishi hawajui nini wanaandika ndio tatizo lao

    ReplyDelete
  4. Hii Naiona Tz pekee Timu Haijamaliza kiporo chake cha Raundi Ya kwanza Anakwenda kucheza mechi Nyingine raundi ya pili

    ReplyDelete
  5. Sasa Leo ndiyo Saleh Jembe mtajua maana ya kupeleka maumivu kwa watani wa jadi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic