KOCHA mkuu wa Alliance FC, Malale Hamsini amesema atatibua rekodi ya Azam FC ya kutofungwa kwenye Uwanja wao wa Chamazi kwenye michezo aliyosimamia mholanzi Hans Pluijm katika mchezo wa leo.
Mpaka sasa Pluijm ameongoza kikosi chake katika michezo 13 Uwanja wa Chamazi bila kufungwa ambapo alishinda michezo 10 ya Ligi Kuu Bara na kutoa sare mchezo mmoja huku michezo miwili ya kombe la Shirikisho akiibuka kidedea.
Malale amesema kuwa :-"Naitambua Azam FC kwa sababu nilicheza nao kabla sijaja hapa Alliance na nilifungwa, nimejifunza mengi na mpaka sasa nina uhakika wa kupata matokeo katika uwanja wao ambao wanauita machinjio.
"Kila timu ina mipango na malengo kwa mwendo ambao kikosi changu chenye vijana wengi wenye juhudi na ari ninaamini nitaushangaza ulimwengu wa mpira, hivyo sapoti ya mashabiki tunahitaji pamoja na kuwataka waamuzi wafuate sheria 17 za mpira.
Kocha wa Azam FC, Hans Pluijm amesema anatambua ugumu uliopo kwenye ligi kutokana na ushindani ia anawaamini wachezaji wake kutokana na mazoezi aliyowapa pamoja na ari waliyonayo wana uhakika wa kupata matokeo.
0 COMMENTS:
Post a Comment