KOCHA mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema wamejipanga kiasi cha kutosha kuutumia vema uwanja wa nyumbani kuipapasa timu ya Ruvu Shooting ya Masau Bwire.
Coastal Union wataikosa huduma ya mchezaji Issa Abushehe ambaye alipewa kadi nyekundu katika mchezo wao waliocheza na Yanga na uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Mgunda amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa leo na tayari amewapa mbinu kali wachezaji wake li kupata matokeo.
"Tupo uwanja wa nyumbani ni nafasi yetu kutumia vema hilo nimewaambia wachezaji uwezo wa kushinda ni ndani ya dakika tisini na wasiwe na presha kila kitu kinawezekana.
"Makosa yaliyopita tumefanyia kazi na nina imani tutaonyesha ushindani wa kweli licha ya wapinzani wetu kutafuta matokeo nasi pia tunahitaji pointi tatu, mashabiki watupe sapoti," amesema Mgunda.
0 COMMENTS:
Post a Comment