MSHAMBULIAJI wa Simba raia wa Rwanda, Meddie Kagere ambaye ana mabao saba kwenye Ligi Kuu kwa sasa, amesema dawa pekee ya kuishusha Yanga kileleni ni ushindi.
Yanga inaongoza Ligi Kuu Bara kwa sasa wakiwa na pointi 55 huku Simba ikiwa nafasi ya tano baada ya kucheza michezo 14 na kujikusanyia pointi 33.
Kagere amesema kuwa kitu pekee ambacho kinawapa nafasi wapinzani wao kuwa vinara ni kutokana na ushindi ambao wanaupata katika michezo yao hivyo nao wanatakiwa kushinda.
"Wachezaji tunajua kwamba siri pekee ambayo itasaidia timu yetu kuongoza Ligi Kuu Bara na kufikia malengo yetu ni kushinda michezo yetu yote ya ligi.
"Wao wamefanikiwa kupata matokeo na ndio maana wanaongoza sisi hatuna wasiwasi kwa sababu tunajua ili kupata pointi ni lazima tushinde ni muda wetu sasa kushinda michezo yetu," alisema Kagere.
Leo Simba watakuwa na mchezo Uwanja wa Taifa dhidi ya Mwadui FC,wakiwa na kumbukumbu kwenye mchezo wao wa mzunguko wa kwanza walishinda mabao 3-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment