MEDDIE kagere mshambuliaji wa Simba jana dakika ya 71 akimalizia pasi ya Bocco alibadilisha mambo manne kwa wakati mmoja baada ya kufunga bao la ushindi Uwanja wa Taifa.
Kagere alibadilisha matokeo kwa kuipa pointi tatu muhimu timu yake na kuifanya ifanikiwe kushinda mchezo wake wa ugenini na kuwa na pointi 39 kutoka 36.
Matokeo hayo pia jambo la pili ni kuifanya Simba ipande kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya tano mpaka kufikia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.
Jambo la tatu ni kuongeza idadi ya mabao ya kufunga awali Kagere alikuwa na mabao nane na sasa anafikisha mabao tisa.
Jambo la nne ni kuongeza idadi ya michezo kwa Yanga ya kupoteza kwani katika michezo yao ya awali walifungwa mchezo mmoja kati ya michezo 23 na jana wanafikisha mchezo wa pili kupoteza.
Kipeke naipongeza ngome ya Yanga kwa kucheza kwa nidhamu na kujituma, pia Mrisho Ngassa alikua na pasi za hatari sana........hongera simba
ReplyDeletePia nampa hongera Julio kwa utabiri wake kuwa Simba ingefungwa na yanga na iliobakia hivi sasa. Julio achukue mikoba ya Marehemu Sheikh Yahya Husein ya utabiri
ReplyDeleteAna hasira zisizomsaidia kitu, utabiri was hasira, kufikiri kwa hasira pia. Ukocha wake umeishia wapi Kyle Dodoma
ReplyDeleteWale wooote waliokuwa wanaitabiria Simba kufungwa, tangu jana jioni siwaoni humu, leo yenyewe imekuwa shwari tu, hata tunaposoma Comments humu ndani, tunasoma kistaarabu tu. Hakuna matusi wala lugha chafu. Leo nimegundua, kumbe wasomaji wa Blog hii ambao huwa wanatoa comments za matusi na lugha chafu ni wa Yanga!. Hakia Mungu Salehe, hata wewe ukitaka hii Blog yako ipate wasomaji wengi na wasio na matusi, Ombea kila ikicheza Yanga IFUNGWE TU! Blog yako itapendeza sana. Naamini hata wewe umeliona hilo.
ReplyDelete