February 17, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga umeanza mikakati kabambe ya kuboresha mkataba wa mchezaji wake, Mshambuliaji Ibrahim Ajibu ambaye ameanza kuhusisha kurejeshwa Simba, imeelezwa.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema hivi sasa kinachoumiza ni kuona namna gani mabosi hao wanafanikisha mipango ya kumbakisha mchezaji huyo fundi.

Kutokana na Yanga kuwa kwenye wakati wa mpito hivi sasa, kuna namna inafanyika ili kupata fedha za kuongeza mkataba wake ili asiondoke na akaelekea alipotokea.

SImba ambao wametoka kuiangamiza Yanga jana kwa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, inaelezwa wameshaanza harakati za kimyakimya kumalizana naye mapema baadaye.

Simba wanaonesha dhahiri shahiri bado wanamkubali Ajibu kutokana na kiwango chake hivyo endapo Yanga watazubaa anaweza akarejeshwa Unyamani.'

Wakati huo Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amezidi kuwaasa Yanga wafanye kila liwezekanalo ili kumbakiza nyota huyo.

Taarifa zinasema Zahera bado anamkubali zaidi mchezaji huyo na anahitaji zaidi huduma yake kwani amekuwa na msaada mkubwa zaidi kikosini.

Takwimu zinaonesha Ajibu tangu ajiunge na Simba misimu miwili iliypita amefunga jumla ya mabao 13.

4 COMMENTS:

  1. Simba Wakitaka Kumrejesha Yanga Hawezi Kuzuia Kwakuwa Nina Imani Ajibu Mwenyewe Atakuwa Amemiss Sana Msimbazi Akifikiria Wale Akina Mkude Wanavyo Tanua Na Kula Bata Simba. Kilicho Mponzaga Ilikuwa Tamaa Maana Wakati Huo Simba Ilikuwa Bado Kwenye Uvutano Wa Uwekezaji Wa Mo, Yanga Wasiwe Na Presha.

    ReplyDelete
  2. Kapewa ukepteni ili asiwe na dhamiri ya kurejea nyumbani. Wakale walisema " mwenda tezi na homu hurejea ngamani. Huwezi kumziwia mtoto kurejea alipokulia na pia kama hunijui jaribu" Ajibu alihamia yanga kutazama maisha yakule na bila ya shaka kagundua ni bora arejee nyumbani kulikonona"

    ReplyDelete
  3. Simba wakimwakimtaka Ajibu Yanga hawawezi zuia kwani hapana hela ya kuweza kumlipa Ajibu!

    ReplyDelete
  4. Na ninahisi ukiachana na Ajibu, karibu robo tatu ya kikosi cha Yanga wanaelekea kumaliza mikataba yao. Na kama watashindwa kumbakiza Ajibu peke yake, wataweza kusajili wachezaji wengine wapya au MAPRO? Haya acha tusubiri tuone, labda atatokea NUHU wa Yanga.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic