MTANANGE kati ya watani wa jadi, Simba na Yanga umemalizika kwa watoto wa Jangwani Yanga kupokea kichapo cha Goli 1 - 0.
Goli la Simba limewekwa Kimiani na Straika wao, Meddie Kagere, dakika ya 71 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Kepteni wake John Bocco.
Baada ya mchezo huo kumalizika Makocha wa klabu zote mbili wamezungumza na waandishi wa habari na kutoa maoni yao juu ya mchezo huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment