February 10, 2019


HESABU zimeanza kwenda kombo kwa mashabiki kutokana na kukata tamaa kwa timu ya Simba kufanya vizuri kimataifa kutona na kuboronga mechi zake za awali.

Nikukumbushe kwamba sasa Simba imecheza michezo mitatu hatua ya makundi ambapo ilishinda mchezo mmoja dhidi ya JS Saora na kupoteza mbele ya AS Vita na All Ahly zote kwa kufungwa mabao matano.

Hilo ni gumu kwa sasa kulikubali kwenye akili za mashabiki pamoja na wachezaji ila ni kweli yametokea sasa kinachotakiwa kufanyika ni mapinduzi ya nguvu.

Wachezaji wa Simba sasa ni muda wa kufuta maumivu kwa mashabiki na taifa kiujumla, ni michezo miwili yote mmeambulia kipigo inaumiza ingawa ni mpira.

Kwa sasa kama ambavyo mlikuwa mmepanga awali mtapigana kufa na kupona kubeba pointi uwanja wa nyumbani hapo inabidi mshikilie.

Ukitazama timu nyingi zinajivunia nyumbani kutokana na kuzoea mazingira pia uwepo wa mashabiki unaongeza nguvu ya kutafuta matokeo.

Muda wenu sasa kutumia mashabiki wenu na uwanja wenu yaliyopita yote mnapaswa msahau kabisa anzeni upya, inawezekana na mtafanikiwa endapo mtakuwa kitu kimoja.

Mabao matano mliyofungwa na AS Vita nchini Congo kabla ya kurudia tena matokeo hayo kwa Al Ahly ya Misri yawe ni somo kwenu lenye maana ya kuleta mabadiliko.

Benchi la ufundi litazame kwa ukaribu mapungufu ambayo yamesababisha kufungwa na kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo jambo litakalosaidia kuleta ari mpya.

Wachezaji mkiwa ndani ya uwanja kila mmoja afanye kazi yake ipasavyo bila kuzembea kwani hicho ndicho kinachowaponza mara zote.

Tabia ya kukabia kwa macho kwa wachezaji wa Simba inatakiwa iachwe mara moja bali vitendo vitumike uwanjani hali itakayosaidia kupata matokeo.

Kumbukeni mnawakilisha Taifa kwenye mashindano ya kimataifa kitakachosaidia kurejesha matumaini ni ushindi kwenu hali itakayorejesha furaha kwa mashabiki.

Endapo wachezaji watafanya kazi kwa vitendo na kucheza kwa juhudi mechi za marudiano kwenye uwanja wa nyumbani uwezekano wa kurudisha mabao matano tuliyofungwa upo.

Kama wao wameweza nyumbani kwao kwa nini sisi tushindwe? Basi sasa ni wakati wetu kujipanga upya kutafuta njia ya kutokea kwani hapa tulipo sio sehemu salama kwetu.

Kitu pekee kitakachotuweka sehemu salama ni kupata matokeo chanya yatakayotupa nguvu ya kusonga mbele zaidi ya hapa tulipo.

Nikigeukia upande wa Ligi Kuu Bara bado naona ushindani unazidi kuimarika taratibu hili ni jambo la msingi hivyo timu zote zinapaswa zitambue kikubwa ambacho mashabiki wanahitaji ni matokeo.

Kila timu inapoingia uwanjani ni lazima kupambana kwa hali na mali kupata matokeo bila ya kujali wanacheza na timu gani.

Mzunguko wa pili timu zote zinapswa zitambue ni muda wa mavuno kwani bingwa wa kweli safari yake inaanza mzunguko huu hivyo mwenye kisu kikali ndiye atakula nyama.

Tunahitaji kumpata mshindi bora ambaye atakuwa mwakilishi wetu kwenye mashindano ya kimataifa na kinachotakiwa ni kushindana kweli bila kuzembea.

Waamuzi msitibue mambo hasa katika michezo ambayo mnachezesha sheria 17 za mpira ni muhumu kuzingatia hali itakayosaidia kuwa na ligi yenye ushindani.

Kutoka Championi

2 COMMENTS:

  1. mfumo wa kocha mbovu 3-5-3 au 4-3-3 ndo utaiokoa simba na sio 4-4-2

    ReplyDelete
  2. Rejesha makanda nyuma Simba na Elmasry walipofungwa magoli mawili laini hapa nyumbani nakuishia simba kwenda kuteseka Egypt. Ukifuatilia timu zetu za nyumbani siku zote zinakosa umakini katika dakika za mwanzo za mchezo zinapocheza na timu za nje na nadhani hata hizo timu za nje pia zinaufahamu wa kutosha juu ya udhaifu huo kwa tumu zetu. Ni tabu sana kuona wachezaji au timu za kitanzania zinapambana kwa lengo la kukomboa magoli wanapotanguliwa kufungwa. Simba ni kiungo na wakidhibitiwa kwenye kiungo mara nyingi huwa hawana mpango mbadala. Ukisikia timu ya Simba ni kiungo wakati huo basi ilikuwa sio rahisi viungo vyao kuzidiwa nguvu kirahisi rahisi tu na timu pinzani . Kwa bahati mbaya sana Simba ya sasa hawapo imara hata kidogo kwenye idara ya ulinzi beki ni ya hovyo. Kisa kikubwa cha wapenzi na mashabiki kupoteza moral ni kutokuwa na imani na benchi la ufundi la timu yao kwa sababu mechi zote mbili Simba walizofungwa mabao kumi 10 watu walipiga kelele sana na kusisitiza chondechonde jamani Simba mnakwenda huko lakini piga ua lakini msije mkaruhusu mabao ya mapema yatawamaliza. Lakini Simba walipokwenda Congo hee? Nnaimani kabisa hata mabao wasingefungwa magoli rahisi na ya aibu kama yale? Sasa watu kwanini wasikereke? Wachezaji wanalipwa vizuri,kocha wa gharama,Simba kupanda ndege au kulala hotel ya nyota tano ni vitu vya kawaida lakini wametolewa kwenye kombe la azam FA kizembe na timu ambayo haijawahi hata kusafiri kutoka nje ya Tanzania. Wakaja kutolewa sport pesa kizembe vile vile kwa wachezaji kutoonesha bidii ya kazi yao. Hatukatai Simba kufungwa na timu tunazoziita kubwa barani Africa lakini sio kufungwa goli tano za kizembe namna ile kwani inaleta au kuieka timu kwenye taswira mbaya kana kwamba wameingia hatua ya makundi kwa kubahatisha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic