February 10, 2019


KOCHA mkuu wa Alliance FC, Malale Hamsini amesema mbinu zake zimekubali na wachezaji wameanza kucheza kwa maelewano wakiwa ndani ya Uwanja hivyo wapinzani wake KMC leo wajipange.

Hamsini alitua Alliance Novemba 24 baada ya kutimuliwa Ndanda kwa kile kilichoelezwa ni matokeo mabovu ameonyesha maajabu kwenye soka baada ya kuongoza michezo sita bila kupoteza na kuipandisha timu kutoka nafasi ya 17 mpaka nafasi ya nane.

Hamsini amesema katika ulimwengu wa mpira hakuna kitu cha kujificha,mwenye uwezo na mbinu ndiye ana uhakika wa kuibuka na ushindi bila kujali atakuwa ugenini ama nyumbani.

"Tayari wachezaji wangu wameona umuhimu wa kucheza kwa kujituma na kutumia uwezo wao wote walionao, nina waamini wanaweza kuushangaza ulimwengu wa soka hasa kwa kupata matokeo katika mechi za ugenini ambazo tunacheza kwa sasa.

"Ushindani ni mkubwa na kila mmoja anahitaji matokeo, vijana wana moto wa kupata ushindi na ndio maana wanaweza kupindua matokeo muda ambao siutarajii," amesema Hamsini.

KMC na Alliance zitacheza leo Uwanja wa Uhuru ikiwa ni mchezo wa marudio na KMC wakiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 2-1 walipocheza mchezo wao wa kwanza mkoani Mwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic