BODI YA LIGI YAJA NA TAMKO LINGINE JUU YA MDHAMINI MKUU LIGI KUU BARA
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mguto, limesema mpaka sasa bado linafanya jitihada za kumpata mdhamini mkuu wa ligi.
Ikumbukwe tangu kuanza msimu wa 2018/19 TFF imekuwa ikisema inaendeleza harakati za kumpata mdhamini huyo lakini mpaka sasa hakuna mafanikio yaliyoonekana.
Mguto amesema wanajitahidi kadri ya uwezo wao kama chombo mama cha soka la Tanzania kuhakikisha wanampata kabla ligi haijamalizika.
Ameeleza kumekuwa na changamoto kubwa lakini hawakati tamaa wakiendelea na mapambano ya kufanikisha azimio hilo.
Haijajulikana hadi leo mshindi wa taji la Ligi Kuu Bara atapata nini kwasababu ya kukosekana mdhamini tangu kujiondoa kwa Vodacom ambao walikuwa wadhamini wa siku nyingi.
0 COMMENTS:
Post a Comment