February 28, 2019


Real Madrid imeendelea kuwa mdebwedo kwa FC. Barcelona baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 katika mchezo wa Kombe la Mfalme usiku huu.

Madrid iliyokuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu imeruhusu kichapo hicho na kuongeza uteja dhidi ya wakali hao wa Catalunya.

Mabao ya Barcelona yamewekwa kimiani na Luis Suarez aliyefunga mawili na moja likiwa la penati.

Mbali na Suarez kutupia mbali, Raphael Varane naye alijifunga akiwa katika harakati za kuokoa na kuizawadia Barcelona bao.

Katika mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa Camp Nou, timu hizo zilenda sare ya bao 1-1.

Matokeo hayo sasa yanaifanya Barcelona kutinga fainali ya michuano hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic