KOCHA MBEYA CITY ASHINDWA KUWAVUMILIA MASHABIKI
Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara jana, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Nsanzurwimo Ramadhan amewachana mashabiki wa timu yake.
Hatua hiyo imekuja kutokana na matokeo ya hivi karibuni ambayo yamekuwa hayawafurahishi hivyo kufikia hatua ya kutupiwa lawama na kulitukana benchi la ufundi.
Amesema mashabiki wa timu yao wamekuwa hawana uchungu na kutoonesha uzalendo wa kuishabikia Mbeya City inapofanya vibaya kitu ambacho kimesababisha mpaka waanze kutukana.
Ramadhani ameelezea suala hilo kuwa kero huku akifunguka kuwa timu inapofanya vibaya si kwamba iache kuungwa mkono bali juhudi za hamasa ziendelee.
Baada ya ushindi wa jana dhidi ya Singida, Kocha Ramadhani ameshauri kuwepo na ustaarabu na utamaduni wa kuheshimu benchi la ufundi kufanya kazi yake na si kutukana.
Jamani huyo katika picha ndie kocha wa Mbeya City??
ReplyDelete