February 11, 2019


Kwa mujibu wa takwimu za mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ambazo zimechezwa mpaka sasa, Emmanuel Okwi yuko vizuri.

Takwimu hizo za Caf, ni za asisti za mechi za makundi yote ya michuano hiyo msimu huu wa 2018/19.

Anayeongoza kwa asisti mpaka sasa ni Tresor Mputu wa TP Mazembe mwenye nne, akifuatiwa na Hussein El Shahat wa Al Ahly ambaye anazo tatu.

Okwi na wachezaji wengine sita wa klabu mbalimbali inaonyesha kwamba wametengeneza asisti mbilimbili mpaka sasa.

Straika huyo wa Uganda ndiye mchezaji pekee wa Simba aliyeko kwenye listi hiyo ya asisti.

Simba yenye pointi tatu kwenye kundi lake, inarudiana na Ahly Jumanne hii jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic