February 11, 2019


BONDIA Cosmas Cheka ametamba kumlaza chali dakika ya kwanza, Emmanuel Bariki ‘Chuga Boy’, watakapovaana katika pambano lao la uzito wa Batam KG 63 la raundi nane litakalofanyika Machi 2, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Msamvu Pub mjini Morogoro.

Cheka amesema kuwa atahakikisha anamkalisha mapema kutokana na kumuona na majigambo mengi huku akisahau kuwa anakutana na mtoto wa mjini Morogoro.

Mratibu wa ngumi hizo, Kaike Silaju, amesema wakati anazungumza na Cosmas Cheka amemkariri akisema kuwa, Machi 2, anaenda kumlaza mapema tu kwa kumpiga KO Chuga Boy na baada ya hapo atakuwa ametoa salamu kwa wengine wote waonajigamba dhidi yake.

“Pambano hilo litakuwa la pili kwa ukubwa kabla ya lile la Kiduku na Maugo kuanza maana tumezingatia zaidi upinzani wao na Chuga Boy hivyo tuna imani kabisa kila atakayepata fursa ya kuingia siku hiyo ataweza kupata burudani kama alivyokusudia,” alisema Silaju.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic