Aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura anatarajia kupandishwa kizimbani leo baada ya kushikiliwa na Takukuru.
Wambura anashikiliwa kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha wakati akiwa madarakani.
Taarifa zinasema anaweza kupandishwa kizimbani leo kujibu tuhuma hizo zinazomkabili baada ya Takukuru kuwa wamefanya kazi yao.
Taarifa zinaeleza, Wambura anashikiliwa kwa siku ya pili baada ya kuwa amehojiwa mara kadhaa.
Hivi karibuni, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) lilitangaza kumfungia Wambura maisha kujihusisha na soka.
0 COMMENTS:
Post a Comment