February 14, 2019


KWA sasa klabu ya soka ya Simba itakuwa ni bandika bandua mpaka kieleweke ili kwenda sawa na timu nyigine kwenye Ligi Kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa sasa Simba imeanza maandalizi ya mchezo wake wa ligi dhidi ya watani zao Yanga, ambao utapigwa Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Baada ya hapo ni safari Jumapili Arusha ambapo itafanya mazoezi kwa siku moja kabla ya mechi yake dhidi ya African Lyon itakayopigwa tarehe 19 Uwanja wa  Sheikh Amri Abeid.

Itarejea Dar es salaam na kujianda kwa siku moja kisha  tarehe 22 itamenyana na Azam FC na kusafiri kwenda Iringa na itakuwa na siku mbili za mazoezi ambapo itacheza tarehe 26 dhidi ya Lipuli FC.

Baada ya mchezo huo itaunganisha Shinyanga na itakuwa na siku mbili tu za mazoezi kabla ya Machi 3 kuivaa Stand United ambapo baadaye itarudi Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya safari ya kwenda Algeria Machi 6 kwenda kucheza na JS Saoura Machi 9.

Simba inashika nafasi ya pili kwenye Kundi D ikiwa na alama sita nyuma ya Al Ahly yenye alama saba huku JS Saoura wakishika nafasi ya tatu wakiwa na alama tano na AS VIta wakishika mkia wakiwa na alama nne.

10 COMMENTS:

  1. Ratiba ya kawaida tu Hanna ilikokaza na ikibidi nyingine zitasogezwa mbele

    ReplyDelete
    Replies
    1. wakimfunga Yanga wataenda kwa ndege wakifungwa kwa basi

      Delete
  2. Hao ni binaadamu, hapana budi wafikiriwe. Wapate mapumziko ili wafanikiwe katika juhudi zao

    ReplyDelete
  3. Bodi yetu ya ligi haijitambui, ratiba hii ni fair kulingana na bodi pamoja na club ya simba kuamua kuweka viporo vingi unnecessarily

    ReplyDelete
  4. da hata fifa wakipelekewa hii ratiba nadhani bodi itahojiwa hawajui kwamba simba ni jina tu lakini wanaocheza ni binadamu? hapana hapa si fair tena ratiba zenyewe za kusafiri kila mara

    ReplyDelete
  5. TFF haitakiwi kuingia kwenye au kufuata kiherehere cha Yanga na akina Mzee Akilmali kuhusiana na ratiba ya Simba kwenye ligi. Kwanza yanga inafundishwa na zahera ambae ni Kocha msaidizi As vita. Kweli Simba ipo nyuma kiratiba lakini hekima lazima itumike kuhakikisha tatiba ya ligi haivurugi Simba kwenye ushiriki wake wa club bingwa Africa. Kuna wanaolalamika kutaka kuona ratiba inakuwa sawa na kuna wale wanaopiga kelele kwa kisingizio cha ratiba kutaka kuona Simba inafanya vibaya hasa kwenye mechi zake za kimataifa. Huwezi kulinganisha mazingira ya mechi za Ahly au js Saoura kwenye ligi ya Egypt au Algeria na ushiriki wao wa club bingwa Africa halafu ulinganishe na Mazingira ya mechi za Simba kwenye ligi ya Tanzania halafu tuitarajie Simba kufanya vyema kwenye mechi zake zilizosalia kwenye club bingwa Africa. Kwanza ifahamike wazi kwamba simba kuwa nyuma katika ratiba ya ligi sio kosa lao. TFF na bodi ya ligi imekiri kuwa mashindano ya sports pesa na kombe la mapinduzi ni moja kati ya mambo yaliochangia kuvurugika kwa ratiba sasa vipi leo ionekane kama Simba ndio wanaopanga ratiba?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uongozi wote wa Tifutifu ni wanazi wa Simba,so wanaitengenezea mazingira ya kupanga matokeo kwenye mechi zake za viporo...

      Delete
  6. Sitaki kuongeza lolote.Umegota kwenye kiini haswa.

    ReplyDelete
  7. Hii ligi hii na ratiba hii hee tusubiri tuone!

    ReplyDelete
  8. Tunadanganyana Kusema Wanaenda Arusha Wakt Swala Liko Wazi tayar Lyon Wameshaomba Mechi Iamishiwe Dar Hvyo Tifua Tifua Wanasubiria Siku Zisogee Tu Watangaze Maamuzi ya Kuwakubalia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic