February 14, 2019



KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa kwenye mechi zao za mzunguko wa pili wanakabiliana na ugumu wa hali ya juu kutokana na kupambana na zaidi ya timu moja uwanjani.

Kocha huyo hadi sasa ameiongoza Yanga kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 58 baada ya kucheza michezo 23.

Kocha huyo Jumamosi hii ataiongoza Yanga kwenye ‘Kariakoo Derby’ kupambana na wapinzani wao wa jadi, Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Zahera amesema mechi zao za awamu hii zinakuwa ngumu kutokana na wapinzani wao wengine kuzicheza kwa kutumia timu ambazo wanapambana nazo.

Pamoja na kwamba Zahera hakutaja moja kwa moja lakini hapa anamaanisha kuwa Simba na timu zingine za nafasi za juu zimekuwa zikihujumu mechi zao kwa kuwa ndiyo wapinzani wao wakubwa kwenye ligi.

5 COMMENTS:

  1. Yanga wapambane na hali yao, waache kutafuta visingizio. Nani asiyejua jinsi Yanga wanavyoihujumu Simba? Muosha huoshwa.

    ReplyDelete
  2. na wewe saleh ni mchonganishaji huwezi kuandika kwamba 'hv ndivyo yanga wanavyohujumiwa ligi kuu'utafikiri umefanya research umeona ni kweli, zahera alikuja hajui siasa na na yeye kaingia mle mle mbona mzungu wa simba habwajuki bwajuki huyu mkongo ni mwanangonjera au ni kocha? sasa katwaa vyeo vyote yanga michango kuchangisha zahera, usemaji wa club zahera, ukocha zahera, uongozi wa club zahera, zahera nikupe pole ebu mwambie Hans van plujin alichofanyiwa, hv unawajua vizuri wabongo hujiulizi kwa nn viongozi wa yanga hata kama ni wachache sasa hv hawazungumzi chochote kuhusu club? maana wewe umetwaa mamlaka yote yanga sasa onyo; Dawa yako inachemka utawajua wabongo kwa nn waliitwa wabongo wewe bwabwaja sasa

    ReplyDelete
  3. Walipocheza mechi 11 mfululizo nyumbani hukusema lolote.Sasa mambo yameanza kukaza ohh wanahujumiwa. Acha ukanjanja na mapenzi ya wazi.Andika ukweli.Call a spade a spade and not a big spoon.
    PUKACHAKA.

    ReplyDelete
  4. Miaka yote ubingwa wa lingi kuu Tanzania bara hauchukuliwi na timu maskini.

    ReplyDelete
  5. hao yanga wapambane na har zao2 sisi tulipitia an hayo kpndkile tukaitw majna kam yote

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic