REKODI ZA SIMBA CAF ZAFURAHISHA KINOMA, HEBU CHEKI HAPA
REKODI za Shirikisho la Soka la Africa(Caf) zinaonyesha kwamba Simba imekuwa na rekodi nzuri katika mechi zake za Ligi ya Mabingwa wanazocheza nyumbani.
Katika michezo 19 ya mwisho ya Ligi ya michuano hiyo ambayo Simba imecheza nyumbani katika misimu tofauti ikiwa ni pamoja na ule wa juzi dhidi ya Ahly imefanya vizuri. Imepoteza mitatu tu, lakini imeshinda mechi 13 na mingine mitatu iliyosalia ilikuwa sare ndani ya Uwanja huo wa Taifa.
Tathmini ya jumla inaonyesha Simba katika siku za hivi karibuni kwenye mashindano yote, imepoteza mechi tatu tu kati ya kumi. Juzi Jumanne iliwafunga Ahly na kufi kisha pointi sita kwenye kundi lake ambazo zimewaweka
kwenye nafasi ya pili katika msimamo wakiwa na pointi sita.
Ahly hawajashinda kwenye mechi zao sita mfululizo walizocheza ugenini ikiwemo ya Simba juzi. Wametoa sare mbili na kupoteza mechi nne huku kisingizio kikiwa hali ya hewa na majeruhi.
Ndo Watajua Nao " Wakitupeleka Kwenye Friji Na Sisi Tuna Wapeleka Kwenye Tanuri La Moto Tuone Nani Jeur"i
ReplyDelete