February 21, 2019


BEKI mkongwe wa Yanga, Kelvin Yondani 'Cotton' amewaambia Simba waendelea kuchonga, lakini wataonana mwishoni mwa msimu wa Ligi Kuu Bara nani ataibuka bingwa.

Kauli hiyo, ameitoa wakati timu hiyo ikiwa kwenye kambini mkoani Mwanza ikijiandaa na mchezo wao wa ligi dhidi ya Mbao FC uliotarajiwa kupigwa jana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Yanga inaongoza kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 58 wakifuatiwa na Azam FC wenye 49 huku Simba wakifuatiwa na 42.

Akizungumza na Spoti Xtra, Yondani alisema; “Sisi hatuna presha kabisa ya ubingwa wa ligi, tunafahamu Simba watateleza na kupoteza michezo inayofuata ya ligi na hilo linawezekana kwao, kwani ngumu kucheza michezo nane bila ya kupoteza.”

“Uzuri wetu sisi tayari tulipata matokeo mazuri katika mzunguko wa kwanza wa ligi na kufanikiwa kukaa kileleni tukiamini mzunguko wa pili utakuwa mgumu, hivyo kila timu itapania kucheza ili zibaki katika ligi zile ambazo zipo katika nafasi mbaya ya kushuka.

“Wao Simba watakutana na kibarua hicho kigumu, hivyo basi hivi sasa tunataka kuona tukipata matokeo mazuri ya ushindi katika michezo ijayo ya ligi na mwishoni mwa ligi tutaona nani bingwa sisi au wao,” alitamba Yondani ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba.

4 COMMENTS:

  1. Hatutelezi Amesahau Mwaka Jana Tumechukuwa Ubingwa Kwa Kupoteza Mechi Moja Tu Na Hata Mwaka Huu Itakuwa Hivyo Simba Imeshapoteza Moja Hiyo Imetosha Hatupotezi Tena Ila Wao Wajiangilie Maana Hata Azam Itawafunga Mara 2

    ReplyDelete
  2. historia itajirudia acheze mpira

    ReplyDelete
  3. Huyu naye anaongea pumba....akajibebe na timu yake.Hajacheza game mbili na Azam halafu unajiamanishaje na kuwa bingwa?

    ReplyDelete
  4. Yaani huyu jamaa anaongea nini!. Ina maana kuifunga mbao 2:1 ndo unajipa jeuri ya kuchukua ubingwa!.

    Halafu anaongea anaenda mbele anarudi nyuma. Eti kwa vile sisi tumeshinda mechi zetu zote mzunguko wa kwanza!, kwani hadi sasa Simba imeshamaliza mechi za mzunguko wa kwanza na ukaona uwiano wa Simba na Yanga kwa mzunguko wa kwanza!?.

    Halafu anasema eti, tulijua mzunguko wa pili utakuwa mgumu ndio maana tulishinda mechi nyingi mzunguko wa kwanza, Lakini Simba hawawezi kumaliza mechi nane bila kupoteza. Kwakuwa timu katika mzunguko wa pili zitakuwa ni ngumu kufungika!, halafu tena unasema tunataka sisi tushinde mechi zetu zote zilizobaki. Huku timu ngumu kufungika, halafu unataka ushinde mechi zako zote, lakini Simba unajua atapoteza! Yanga ni nani ishinde na Simba ni ipi isishinde!? Huyu jamaa hayuko sawa, bao moja la Simba bado limemlevya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic