February 21, 2019


KIKOSI cha Simba kitasafiri kwenda Algeria kwa ajili ya kucheza mechi ya marudiano na wenyeji wao JS Saoura katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ile ya kwanza kushinda mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Mechi hii itapigwa Machi 9.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amesema kuwa mechi za ligi ambazo watacheza katika siku za karibuni zitakuwa msaada tosha kwao kwa ajili ya mechi yao hiyo ya kimataifa.

“Tuna ratiba ngumu ya mechi za karibukaribu katika Ligi Kuu Bara ambazo kwetu tunatakiwa kupata ushindi kwa ajili ya kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.

“Lakini nje ya kupata pointi kwenye mechi hizo zote, mechi hizo tunazichukulia kama sehemu yetu ya maandalizi kwa ajili ya mechi yetu ya kimataifa dhidi ya JS Saoura.

Simba ilianza jumanne kwa ushindi dhidi ya African Lyon, Ijumaa itamenyana na Azam FC uwanja wa Taifa kabla ya kuifuata Lipuli ya Matola.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic