Unaweza kusema mambo yanazidi kuwa moto na adhabu zinatolewa kama njugu hasa kwa wale wanaokiuka sheria za mchezo wa soka.
Maana Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake Februari 9, 2019 chini ya Mwenyekiti wake Wakili Kiomoni Kibamba ilipitia mashauri 15 yaliyowasilishwa mbele yake na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, na kufanya uamuzi ufuatao;
Mchezaji Rashid A Shilla wa Mgambo Shooting amefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 38(7) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, faini ilipwe ndani ya siku 30.
Alilalamikiwa kuwa Januari 13, 2019 kwenye mechi dhidi ya Geita Gold FC alimpiga kichwa Meneja wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi wakati timu zinaingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Mtunza Vifaa (Kit Man) Alimu Hadji wa Mashujaa FC amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, faini ilipwe ndani ya siku 30.
Alilalamikiwa kuwa 03/11/2018 katika Uwanja wa Mwakangale, Mbeya akishirikiana na Daktari wa timu yake alivamia uwanja kwenye eneo la kuchezea (pitch) kwa lengo la kutaka kuwapiga waamuzi.
Daktari Adamu Maftar wa Mashujaa FC amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, na faini ilipwe ndani ya siku 30.
Alilalamikiwa kuwa 03/11/2018 katika Uwanja wa Mwakangale akishirikiana na Mtunza Vifaa alivamia uwanja eneo la kuchezea (pitch) kwa lengo la kutaka kuwapiga waamuzi.
Meneja wa Transit Camp, Bw. Moshi Hamisy amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi sita (6) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, na faini ilipwe ndani ya siku 30.
Alilalamikiwa kuwa tarehe 10/11/2018 katika mechi namba 31, kundi B Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Green Warriors iliyofanyika Uwanja wa Azam Complex aliingia uwanjani na kumsukuma mwamuzi.
Kocha Msaidizi wa Transit Camp, Bw. Thomas Gama amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, na faini ilipwe ndani ya siku 30.
Alilalamikiwa kuwa tarehe 10/11/2018 katika mechi namba 31, kundi B Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Green Warriors iliyofanyika Azam Complex alifanya vurugu kwa kutokubaliana na maamuzi aliyoyatoa mwamuzi wa mchezo.
Kiongozi wa Transit Camp, Bw. Santos Kato amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2)ya Ligi Daraja la Kwanza.
Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, faini ilipwe ndani ya siku 30.
Alilalamikiwa kuwa tarehe 10/11/2018 katika mechi namba 31, kundi B Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Green Warriors iliyofanyika Azam Complex alianzisha vurugu na kusababisha mchezo kusimamishwa.
Baadae alipelekwa jukwaa kuu lakini aliendelea na vurugu hizo.
0 COMMENTS:
Post a Comment