February 28, 2019


KAMANDA wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema msanii, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi Oyster Bay jijini Dar es Salaam kwa mahojiano kutokana na tuhuma za kukashifu na kutoa lugha za kejeli kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, marehemu Ruge Mutahaba.

Jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe alilielekeza Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukulia hatua ‘Dudu Baya’ kwa kumdhihaki Ruge ambaye alifariki jana nchini Afrika Kusini.

Lakini baadaye kupitia akaunti yake ya Instagram, Dudu Baya alimjibu waziri huyo na kusema asisumbuke kuwaagiza polisi wamsake kwani watapoteza mafuta bure, badala yake wamuelekeze ni kituo gani cha polisi akaripoti.

1 COMMENTS:

  1. Waziri Mwakyembe anatumia mamlaka yake vibaya na yeye ni mwanasheria nguli. Kwanini Dudu baya kakamatwa? Ametenda kosa gani hata akamatwe? Hajamtukana mtu kwani maneno ya dhihaki sio matusi. Tungeomba mamlaka husika itumuie busara ya kumpa Dudu baya haki yake ya msingi kutoa maoni yake bila ya kubugudhiwa.Hata angekamatwa kwa utata wa jina lake ingemake sense. Kwnini asikamatwe Tundu Lisu anaemtukana kiongozi mkuu wa nchi mchana kweupe kwa kisingizio chake kwamba yeye haitukani nchi bali anamtukana kiongozi wa nchi wakati anafahamu fika yakwamba kiongozi wa nchi ni muakilishi wa watu na nchi bila ya watu ni jangwa sio nchi tena. Wakusakwa na kuakamatwa ni Tundu Lisu sio Dudu baya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic