February 28, 2019


Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amemvaa tena Msemaji wa Yanga, Dismas Ten kuhusiana na picha ya kiungo wa Simba, Said Ndemla aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram.

Ten aliweka picha hiyo ambayo Ndemla alikuwa amevaa jezi yenye rangi ya njano na kuandika "Rangi ya njano kwenye bendera yetu tukufu ya Tanzania ina maana ya kutukumbusha juu ya utajiri wa madini tuliyonayo... Mambo mengi, muda mchache.. Tusubiri joto lipungue".

Kutokana na POSTI hiyo, Manara naye alimjibu namna hii

"Baada ya kukosa kiki kuhusu Uchawi na Madawa Vyumbani,yule yule anaependa kuzua kaja na Porojo nyingine!!

"Guys Hayupo mchezaji kwa sasa anaeweza kuhama Simba akaenda klabu ambayo hawajui Shibe yao ya kesho!!

Puuzeni Takataka zinazoandikwa kimafumbo, Ndemla ni sehemu ya klabu bingwa ya nchi"



5 COMMENTS:

  1. Mm Ni fan mkubwa WA simba ILA kusem ukwel ndemla Ni hazin inayopata kitu...ndemla Ana kipaj n Ni mchezaj mwandamiz but hapew heshim km mkude....hata 30 or 45 min Ni muhim kukaa bench kunapoteza kujiamin

    ReplyDelete
  2. Wachezaji wote hawawezi kucheza kwa wakati mmoja.Bukaba anapata nafasi sasa. Aongeze bidii ili afiti mfumo wa kocha. Ni mchezaji mzuri kwa kushabikia lakini sio kuzuia. Midfielders wanatakiwa wawe na extra quality.

    ReplyDelete
  3. Huyu Dismas hajui kwamba anaweza kushtakiwa kwa kuweka picha ya mchezaji wa timu nyingine kwenye Instagram yake?
    Tena yeye akiwa si shabiki bali kiongozi?
    Simba wanafaa wafikirie kupeleka mashtaka TFF na kama hatua hazichukuliwi FIFA.

    ReplyDelete
  4. Jibu La Manara Lina Tosha Huwezi Kwenda Sehemu Yenye Njaa Kujinusuru Na Njaa Kali So Hakuna Mchezaj Wa Simba Mwenye Ndoto Za Kwenda Jangwani Kwenye Njaa

    ReplyDelete
  5. Duuh! wengine wawe wanakaa kimya tu!, Sasa Ten nae kwasasa anaongea nn!. Angalia hata LIKES (TEN - Likes 45) ? (MANARA / KAMANDA - Likes 8,893). Hivyo hivyo ndivyo hata mwisho wa msimu watakavyotofautiana ubora wa timu na wingi wa points.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic